Sunday, March 6, 2016

TANZIA

MZEE ABEL SHENKALWA MGONDA. 1928-2016

Ukoo wa Mgonda kwa mshituko mkubwa tunapenda kutoa taarifa ya Kifo cha Baba yetu Mzee Abel shenkalwa Mgonda. Kilichotokea tar 28 Februari 2016 Usiku katika Kituo cha Afya Mlalo na kuzikwa tar 29 Februari 2016.Nyumbani kwake Ngwelo Mission.
Mzee abel amezaliwa mwaka 1928 huko Mtae Kweviama.Yeye ni Mtoto wa tano wa Babu yetu Shekiboko.
Bwana ametoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

TUKIO LA MAZISHI LITAWAJIA.............

Tuesday, September 29, 2015

TENDO LA KIPAIMARA

MATUKIO KATIKA PICHA























KIPAIMARA LOVENESS & GODBLESS

Tarahe 19.7.2015 imekuwa siku ya furaha sana kwetu familia ya mgonda kwa watoto wetu Mapacha kupata kipaimara.katika Usharika wa Takorora Tanga.
Hapa waweza ona matukio katika picha
 Mhe Askofu Rev Dr Munga akihubiri neno la Mungu
Rev Dr E.Ngugi akitoa salam

 
Kwaya ya vijana ikisifu ibadani
 


 Gobless akiwa katika ibada
Lovenes na wenzake wakiwa katika maandamano wakitoka idabani

Thursday, March 5, 2015

HERI WENYE MOYO SAFI

Ni maneno ya kutiana Moyo wakati shida huzuni  na Ugonjwa
Mungu huangalia moyo wa kila mtu katika shida yake na maombi yake kwa Mungu wetu.
Tumeona baraka kubwa kuwa pamoja kama inavyoonekana tar za mwanzo mwaka huu 2015 tukiwa na mgeni wetu toka ujerumani Bi Andrea aliye mgeni wa usharika wa Ngwelo







Pamoja tumefurahi

Wednesday, September 12, 2012

Wednesday, August 22, 2012

HISTORIA YA UKOO WA MGONDA WA SHEKIBOKO

 MZEE ABEL MGONDA SHENKALWA

HISTORIA YA UKOO WETU MGONDA (SHENKALWA)

Nimejaliwa kufanya mahojiano na mzee Abeli Mgonda juu ya ukoo wetu wa Mgonda tar 13.08.2012 nikiwa likizo Ngwelo .Baada ya kusafiri kwenda Mtae na  kufika eneo la Kweviama ambako babu yetu Shekiboko ndipo alipokuwa na makazi yake na kuwazaa watoto wake wapatao kumi.(10)

KUMBE UKOO WETU ULITOKANA WAZEE HAWA
Babu yetu  anaye wazaa baba zetu anaitwa SHEKIBOKO, ambaye amazaliwa na ndugu zake wanne ambao ni
  • Shekiondo
  • Mtambo (ambaye alipiagana vita vya kumi na nne akiwa askari Kea)
  • Mamunga (Mwiuwa) Ke
  • Mbughu  Ke
Jumla ya Babu na bibi zetu wazaa baba zetu ni watu watano.sijapata  babu hawa wanazaliwa na nani.
 Kwa mujibu wa mzee Abel ukoo huu wote walikuwa wasilamu kama sio wapagani kwa muda huo.
Uzao wa babu yetu akina Mgonda.
Babu Shekiboko alijaliwa kuwa na watoto kumi ambao wote aliwazaa na kukua katika upagani na Uisilamu. Kwa  mujibu wa mzee abel mtoto wa pili wa babu shekiboko aliyeitwa SEMBUA ndiye alibatizwa kwanza na kufanya ndugu zake wengi , baba yake na mama  (Babu na Bibi) yake kubatizwa.hivyo waliobatizwa nitawaja majina yao yote.

Wafuatao ni watoto wa babu Shekiboko Shenkalwa Mgonda
Nafasi
ya kuzaliwa
Jina
Jina la Ubatizo
Mwaka wa kuzaliwa
1
HASSANI (SHEUYA)
Hakubatizwa

2
SEMBUA
LOTH
1922
3
NYANGE
ERNEST

4
MTUTU


5
SHEMBOZA
ABEL
1932
6
MAMGHANGA


7
KIVUI


8
CHONGE



9

NKONDO (Musa)
Alibatizwa  Ngwelo mwaka 1993  na kuitwa Moses

10
KIBADA
YOHANA


MZEE SEMBUA (LOTH) Alibahatika kusoma zamani wakati utawala Wajerumani naye alikuwa mwenye uwezo mkubwa Darasani na Ujasiri na Hekima. Katika kukua kwake. Mjerumani maarufu katika Historia ya Milima ya Usambara katika  kuenea kwa neno la Mungu . anayeitwa Bwana Volapi.
alimpenda sana Baba yetu Sembua.  Baba yetu SEMBUA alifuatilia kwa makini mambo ya kikristo akiwa shuleni  na kuamua kubatizwa akiwa amechagua jina lake aitwe  Gustafu. Mchungaji aliyekuwepo Mtae alikuwa tayari amepewa jina atakaloitwa Mzee SEMBUA (Kijana wakati huo). Baada ya  kumuuliza Sembua jina lako unalopenda kesho (siku ya kubatizwa kwake) alijibu kuwa anataka aitwe Gustafu, Gustafu ni mwalimu katika shule moja hapo Mtae. Mchungaji huyu alimtuma  SEMBUA aende kwa Bwana Volapi. Ambapo Bw. Volapi alimuuliza kwa kisambaa
“ Kumbe mghoshi lushe ushaghule zina ani?"  Sembua alijibu kuwa nataka kuitwa Gustafu. Bw Volapi alimwambia hapana  hapana Jina lako wewe Utaitwa Loth  kwa sababu Mtae ni kama SODOMA na GOMOLA na Wewe utangulie ndugu zako watakufuata.

Bila ubishi kijana SEMBUA alikubali jina hilo na siku iliyofuata alibatizwa na kuitwa Loth. Huu ni kati ya mwaka 1941 na 1942
Aliendelea kukua na kusoma shuleni vizuri. Baraka kubwa aliyopata ni pale mama yake naye alikubali kubatizwa Bibi yetu OHIZA  na kuitwa  Miriam , baadae akabatizwa  mzee nyange aliyeitwa ERNEST na kisha SHEMBOZA  naye akabatizwa  na Kuitwa ABEL na baadae kuingia mafunzo ya kipaimara. Mdogo wao wa mwisho Kibada alibatizwa na kuitwa YOHANA. Mwisho kabisa Babu yetu Shekiboko naye akabatizwa na kuitwa HOKELAI.
Baada ya Babu kubatizwa aliendelea vizuri katika imani ya Kikiristo na kulea watoto wake vema. Akiwa mfugaji na mkulima.
Mwaka 1972 aliitwa mbinguni na baadae mwaka mmoja hivi bibi Miriam naye aliitwa mbinguni.

Kwa shukrani za pekee kwa Mungu ni kuwa tunaye Mzee Abel ambaye sasa ni mzee wa miaka 80 na kitu kwa Mujibu wa maelezo yake anasema katika ukoo  wetu baba/babu aliyebakia ni yeye tu kama reference ,  akadai kuwa yuko mama mmoja dada yake yuko maeneo ya upareni lakini hajulikani sana huku kwetu.mwanae mmoja dada yupo Mtae. Nimefanikiwa kumuona dada huyu.
 
FAMILIA YA KASINDA

Babu mkubwa wa kwanza anayeitwa shekiondo ndiye anayewazaa wazee wetu
BOAZI NA YONA
Yona naye alipigana vita vya kumi na nne.

BOAZI  ndiye anayemzaa kaka yetu marehemu Mganga Tamilwai,Kaka Izai, na Staile

YONA ndiye anayemzaa Pauli, Zephania (Mchungaji),Onai,Mkunde (sara), na Otie


** Katika historia ya ukoo wetu yapo mambo kadhaa yanajirudia kwa mfano

Babu aliyeitwa Mtambo ambaye jina lake baadae alipewa kaka Athumani mtoto wa Mzee Hassani .Huyu Athumani(Mtambo)  naye alipigana vita vya kumng’oa  IDD Amini Dada wa Uganda.   1978-1979**

Aidha kwa Mujibu wa Mzee Abel ukoo wetu  chanzo chake ni katika mji wa Lushoto eneo la Ubiri ambapo baadae ndugu walisambaa katika maeneo mengi ya Lushoto kama Mtae, Mambo ya Mtae,  Dule ya Mlalo na Kwingineko kama ilivyokuwa desturi ya Kabila la Wasambaa.

Itaendelea……….
** Tafadhali kama unayo taarifa/picha yoyote kuhusu ukoo wetu tafadhali nitumie niweke katika Blog yetu. Pia kila mtoto aliyepo sasa anaweza kuweka taarifa zake katika blog hii kwa maufaa ya wengine.
Na mwanafamilia Thomas Mgonda ( Joseph) Email: mgonda5@yahoo.com mobile: 0713600694