Wednesday, September 12, 2012

Wednesday, August 22, 2012

HISTORIA YA UKOO WA MGONDA WA SHEKIBOKO

 MZEE ABEL MGONDA SHENKALWA

HISTORIA YA UKOO WETU MGONDA (SHENKALWA)

Nimejaliwa kufanya mahojiano na mzee Abeli Mgonda juu ya ukoo wetu wa Mgonda tar 13.08.2012 nikiwa likizo Ngwelo .Baada ya kusafiri kwenda Mtae na  kufika eneo la Kweviama ambako babu yetu Shekiboko ndipo alipokuwa na makazi yake na kuwazaa watoto wake wapatao kumi.(10)

KUMBE UKOO WETU ULITOKANA WAZEE HAWA
Babu yetu  anaye wazaa baba zetu anaitwa SHEKIBOKO, ambaye amazaliwa na ndugu zake wanne ambao ni
  • Shekiondo
  • Mtambo (ambaye alipiagana vita vya kumi na nne akiwa askari Kea)
  • Mamunga (Mwiuwa) Ke
  • Mbughu  Ke
Jumla ya Babu na bibi zetu wazaa baba zetu ni watu watano.sijapata  babu hawa wanazaliwa na nani.
 Kwa mujibu wa mzee Abel ukoo huu wote walikuwa wasilamu kama sio wapagani kwa muda huo.
Uzao wa babu yetu akina Mgonda.
Babu Shekiboko alijaliwa kuwa na watoto kumi ambao wote aliwazaa na kukua katika upagani na Uisilamu. Kwa  mujibu wa mzee abel mtoto wa pili wa babu shekiboko aliyeitwa SEMBUA ndiye alibatizwa kwanza na kufanya ndugu zake wengi , baba yake na mama  (Babu na Bibi) yake kubatizwa.hivyo waliobatizwa nitawaja majina yao yote.

Wafuatao ni watoto wa babu Shekiboko Shenkalwa Mgonda
Nafasi
ya kuzaliwa
Jina
Jina la Ubatizo
Mwaka wa kuzaliwa
1
HASSANI (SHEUYA)
Hakubatizwa

2
SEMBUA
LOTH
1922
3
NYANGE
ERNEST

4
MTUTU


5
SHEMBOZA
ABEL
1932
6
MAMGHANGA


7
KIVUI


8
CHONGE



9

NKONDO (Musa)
Alibatizwa  Ngwelo mwaka 1993  na kuitwa Moses

10
KIBADA
YOHANA


MZEE SEMBUA (LOTH) Alibahatika kusoma zamani wakati utawala Wajerumani naye alikuwa mwenye uwezo mkubwa Darasani na Ujasiri na Hekima. Katika kukua kwake. Mjerumani maarufu katika Historia ya Milima ya Usambara katika  kuenea kwa neno la Mungu . anayeitwa Bwana Volapi.
alimpenda sana Baba yetu Sembua.  Baba yetu SEMBUA alifuatilia kwa makini mambo ya kikristo akiwa shuleni  na kuamua kubatizwa akiwa amechagua jina lake aitwe  Gustafu. Mchungaji aliyekuwepo Mtae alikuwa tayari amepewa jina atakaloitwa Mzee SEMBUA (Kijana wakati huo). Baada ya  kumuuliza Sembua jina lako unalopenda kesho (siku ya kubatizwa kwake) alijibu kuwa anataka aitwe Gustafu, Gustafu ni mwalimu katika shule moja hapo Mtae. Mchungaji huyu alimtuma  SEMBUA aende kwa Bwana Volapi. Ambapo Bw. Volapi alimuuliza kwa kisambaa
“ Kumbe mghoshi lushe ushaghule zina ani?"  Sembua alijibu kuwa nataka kuitwa Gustafu. Bw Volapi alimwambia hapana  hapana Jina lako wewe Utaitwa Loth  kwa sababu Mtae ni kama SODOMA na GOMOLA na Wewe utangulie ndugu zako watakufuata.

Bila ubishi kijana SEMBUA alikubali jina hilo na siku iliyofuata alibatizwa na kuitwa Loth. Huu ni kati ya mwaka 1941 na 1942
Aliendelea kukua na kusoma shuleni vizuri. Baraka kubwa aliyopata ni pale mama yake naye alikubali kubatizwa Bibi yetu OHIZA  na kuitwa  Miriam , baadae akabatizwa  mzee nyange aliyeitwa ERNEST na kisha SHEMBOZA  naye akabatizwa  na Kuitwa ABEL na baadae kuingia mafunzo ya kipaimara. Mdogo wao wa mwisho Kibada alibatizwa na kuitwa YOHANA. Mwisho kabisa Babu yetu Shekiboko naye akabatizwa na kuitwa HOKELAI.
Baada ya Babu kubatizwa aliendelea vizuri katika imani ya Kikiristo na kulea watoto wake vema. Akiwa mfugaji na mkulima.
Mwaka 1972 aliitwa mbinguni na baadae mwaka mmoja hivi bibi Miriam naye aliitwa mbinguni.

Kwa shukrani za pekee kwa Mungu ni kuwa tunaye Mzee Abel ambaye sasa ni mzee wa miaka 80 na kitu kwa Mujibu wa maelezo yake anasema katika ukoo  wetu baba/babu aliyebakia ni yeye tu kama reference ,  akadai kuwa yuko mama mmoja dada yake yuko maeneo ya upareni lakini hajulikani sana huku kwetu.mwanae mmoja dada yupo Mtae. Nimefanikiwa kumuona dada huyu.
 
FAMILIA YA KASINDA

Babu mkubwa wa kwanza anayeitwa shekiondo ndiye anayewazaa wazee wetu
BOAZI NA YONA
Yona naye alipigana vita vya kumi na nne.

BOAZI  ndiye anayemzaa kaka yetu marehemu Mganga Tamilwai,Kaka Izai, na Staile

YONA ndiye anayemzaa Pauli, Zephania (Mchungaji),Onai,Mkunde (sara), na Otie


** Katika historia ya ukoo wetu yapo mambo kadhaa yanajirudia kwa mfano

Babu aliyeitwa Mtambo ambaye jina lake baadae alipewa kaka Athumani mtoto wa Mzee Hassani .Huyu Athumani(Mtambo)  naye alipigana vita vya kumng’oa  IDD Amini Dada wa Uganda.   1978-1979**

Aidha kwa Mujibu wa Mzee Abel ukoo wetu  chanzo chake ni katika mji wa Lushoto eneo la Ubiri ambapo baadae ndugu walisambaa katika maeneo mengi ya Lushoto kama Mtae, Mambo ya Mtae,  Dule ya Mlalo na Kwingineko kama ilivyokuwa desturi ya Kabila la Wasambaa.

Itaendelea……….
** Tafadhali kama unayo taarifa/picha yoyote kuhusu ukoo wetu tafadhali nitumie niweke katika Blog yetu. Pia kila mtoto aliyepo sasa anaweza kuweka taarifa zake katika blog hii kwa maufaa ya wengine.
Na mwanafamilia Thomas Mgonda ( Joseph) Email: mgonda5@yahoo.com mobile: 0713600694

Thursday, July 12, 2012

SEND OFF & WEDDING ELIZABETH

SEND OFF TAR 29.JUNE 2012 UKUMBI POLISI MESS TANGA

Mungu ni mwema sana katika maisha yetu kila siku.Mpendwa mdogo wetu Elizabeth ametimza sehemu ya majukumu yake kama mtoto wa kike katika familia yetu kwa kutuletea Shemeji.ambapo tar 29.06.2012 tukiwa wote kama familia alituonyesha mpendwa wake na baba (Mjomba) Shewali alimkabidhi rasmi kwa familia ya Kagongo wa Kigoma. Jua huanza kutokea Tanga na machweo Kigoma mwisho wa Reli.
Bwana apewe sifa.
 
ELIZABETH AKIWA NA MAPAMBE WAKE

 
ELIZABETH AKIWA NA MCHUMBA WAKE AKIMUONYESHA KWA FAMILIA NA NDUGU NA JAMAA

SHEREHE KWA UJUMLA TANGU NYUMBANI KIBOI 
 
 
 
 
 
 
 

 
 
 
 
 
 
 
Kaka Mch. Mtahafu Kasinda Akiombea shughuli na salam zake kwa waalikwa.


MAMBO YA MISOSI NA KIHENDO
 
 
 
 
 
 
 
Tunaendelea........................................!!!!!!!!!!!

Wednesday, July 11, 2012

KWETU MAGAMBA-KIJIJINI

Hapa Magamba ni Pazuri kuishi vitu vingi vinapatikana  viazi ,mboga zote Ila baridi tu ndio kitu kigumu hapa na vilima vya hapa na pale.Nikiwa hapa Magamba kama mtumishi Nimejaliwa na Mungu kupata plot na kujenga nyumba mbili zenye room 10 kwa Ujumla.Wapendwa wanafunzi wanaishi hapo.

KARIBU KWETU MAGAMBA
 
 
 
Nyumba ya chini yenye milango mitatu ni ya jirani tunayepakana naye.
nyumba yetu ni hizo zenye rangi  na mabomba marefu nje.

TATE LOTH NKANILEKA NA WENGINE

Nafurahi tena kumuona tate Loth kwa upande wa pili wa shilingi.Baba yetu.Barikiwa sana.
Bw. Loth Nkanileka Mgonda
 
 Bw. Godbless Loth Mgonda
 
 
 
 
 Mrs T.Mgonda na watoto wake wakifurahia zawadi zao  x.mass 2010
 
 Loveness na Alice Mgonda Nyumbani kwtu Kiboi Tanga
 Kwetu Pazuri - Kiteghe na miwa Kibao Jiwe kubwa
 
Mr Thomas Mgonda (Joseph)

Tuesday, July 10, 2012

SHEREHE YA KUAGANA MAGAMBA HOUSE

MWAKA 2011
Katika nyumba yetu ya magamba wakazi wetu wanne wamehitimu Degree ya kwanza na kuagwa na wenzao. Sherehe ilifana na ya mfano katika mtaa wetu wa Coast.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
WAAGWA KATIKA PICHA YA PAMOJA
Wakazi wa Magamba House wafurahia siku yao



 
 
 
Bw.Thomas Mgonda akitoa Zawadi kwa wanaoagwa


 
 

 
 
jirani wa karibu katika Furaha yao.Mtaani kwetu