MGONDA FAMILY
SLP 46 NGWELO MLALO LUSHOTO TANGA TANZANIA
Monday, July 10, 2017
Sunday, March 6, 2016
TANZIA
![]() |
MZEE ABEL SHENKALWA MGONDA. 1928-2016 |
Ukoo wa Mgonda kwa mshituko mkubwa tunapenda kutoa taarifa ya Kifo cha Baba yetu Mzee Abel shenkalwa Mgonda. Kilichotokea tar 28 Februari 2016 Usiku katika Kituo cha Afya Mlalo na kuzikwa tar 29 Februari 2016.Nyumbani kwake Ngwelo Mission.
Mzee abel amezaliwa mwaka 1928 huko Mtae Kweviama.Yeye ni Mtoto wa tano wa Babu yetu Shekiboko.
Bwana ametoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
TUKIO LA MAZISHI LITAWAJIA.............
Tuesday, September 29, 2015
KIPAIMARA LOVENESS & GODBLESS
Tarahe 19.7.2015 imekuwa siku ya furaha sana kwetu familia ya mgonda kwa watoto wetu Mapacha kupata kipaimara.katika Usharika wa Takorora Tanga.
Mhe Askofu Rev Dr Munga akihubiri neno la Mungu
Rev Dr E.Ngugi akitoa salam |
Kwaya ya vijana ikisifu ibadani |
Gobless akiwa katika ibada
Lovenes na wenzake wakiwa katika maandamano wakitoka idabani
Thursday, March 5, 2015
HERI WENYE MOYO SAFI
Ni maneno ya kutiana Moyo wakati shida huzuni na Ugonjwa
Mungu huangalia moyo wa kila mtu katika shida yake na maombi yake kwa Mungu wetu.
Tumeona baraka kubwa kuwa pamoja kama inavyoonekana tar za mwanzo mwaka huu 2015 tukiwa na mgeni wetu toka ujerumani Bi Andrea aliye mgeni wa usharika wa Ngwelo
Mungu huangalia moyo wa kila mtu katika shida yake na maombi yake kwa Mungu wetu.
Tumeona baraka kubwa kuwa pamoja kama inavyoonekana tar za mwanzo mwaka huu 2015 tukiwa na mgeni wetu toka ujerumani Bi Andrea aliye mgeni wa usharika wa Ngwelo
Pamoja tumefurahi
Wednesday, September 12, 2012
Wednesday, August 22, 2012
HISTORIA YA UKOO WA MGONDA WA SHEKIBOKO
MZEE ABEL MGONDA SHENKALWA
HISTORIA YA UKOO WETU MGONDA (SHENKALWA)
Nimejaliwa kufanya mahojiano na
mzee Abeli Mgonda juu ya ukoo wetu wa Mgonda tar 13.08.2012 nikiwa likizo
Ngwelo .Baada ya kusafiri kwenda Mtae na kufika eneo la Kweviama ambako babu yetu Shekiboko ndipo alipokuwa na makazi yake
na kuwazaa watoto wake wapatao kumi.(10)
KUMBE UKOO WETU ULITOKANA WAZEE HAWA
Babu yetu anaye wazaa baba zetu anaitwa SHEKIBOKO, ambaye amazaliwa na ndugu
zake wanne ambao ni
- Shekiondo
- Mtambo (ambaye alipiagana vita vya kumi na nne akiwa askari Kea)
- Mamunga (Mwiuwa) Ke
- Mbughu Ke
Jumla ya Babu na bibi zetu wazaa
baba zetu ni watu watano.sijapata babu
hawa wanazaliwa na nani.
Kwa mujibu wa mzee Abel ukoo huu
wote walikuwa wasilamu kama sio wapagani kwa muda huo.
Uzao wa babu yetu akina Mgonda.
Babu Shekiboko alijaliwa kuwa na
watoto kumi ambao wote aliwazaa na kukua katika upagani na Uisilamu. Kwa mujibu wa mzee abel mtoto wa pili wa babu
shekiboko aliyeitwa SEMBUA ndiye
alibatizwa kwanza na kufanya ndugu zake wengi , baba yake na mama (Babu na Bibi) yake kubatizwa.hivyo waliobatizwa
nitawaja majina yao yote.
Wafuatao ni watoto wa
babu Shekiboko Shenkalwa Mgonda
Nafasi
ya kuzaliwa
|
Jina
|
Jina la Ubatizo
|
Mwaka wa kuzaliwa
|
1
|
HASSANI (SHEUYA)
|
Hakubatizwa
|
|
2
|
SEMBUA
|
LOTH
|
1922
|
3
|
NYANGE
|
ERNEST
|
|
4
|
MTUTU
|
||
5
|
SHEMBOZA
|
ABEL
|
1932
|
6
|
MAMGHANGA
|
||
7
|
KIVUI
|
||
8
|
CHONGE
|
||
9
|
NKONDO (Musa)
|
Alibatizwa Ngwelo mwaka 1993 na kuitwa Moses
|
|
10
|
KIBADA
|
YOHANA
|
MZEE SEMBUA (LOTH) Alibahatika
kusoma zamani wakati utawala Wajerumani naye alikuwa mwenye uwezo mkubwa Darasani
na Ujasiri na Hekima. Katika kukua kwake. Mjerumani maarufu katika Historia ya
Milima ya Usambara katika kuenea kwa neno
la Mungu . anayeitwa Bwana Volapi.
alimpenda sana Baba yetu Sembua. Baba yetu SEMBUA alifuatilia kwa makini mambo ya kikristo akiwa shuleni na kuamua kubatizwa akiwa amechagua jina lake aitwe Gustafu. Mchungaji
aliyekuwepo Mtae alikuwa tayari amepewa jina atakaloitwa Mzee SEMBUA (Kijana wakati huo). Baada ya kumuuliza Sembua jina lako unalopenda kesho
(siku ya kubatizwa kwake) alijibu kuwa anataka aitwe Gustafu, Gustafu ni mwalimu
katika shule moja hapo Mtae. Mchungaji huyu alimtuma SEMBUA aende kwa Bwana Volapi. Ambapo Bw.
Volapi alimuuliza kwa kisambaa
“ Kumbe mghoshi lushe ushaghule zina ani?" Sembua alijibu kuwa nataka kuitwa Gustafu. Bw
Volapi alimwambia hapana hapana Jina
lako wewe Utaitwa Loth kwa sababu Mtae ni
kama SODOMA na GOMOLA na Wewe utangulie ndugu zako watakufuata.
Bila
ubishi kijana SEMBUA alikubali jina hilo na siku iliyofuata alibatizwa na kuitwa Loth. Huu ni kati ya mwaka 1941 na 1942
Aliendelea
kukua na kusoma shuleni vizuri. Baraka kubwa aliyopata ni pale mama yake naye
alikubali kubatizwa Bibi yetu OHIZA na kuitwa
Miriam , baadae
akabatizwa mzee nyange aliyeitwa ERNEST na kisha SHEMBOZA naye akabatizwa na
Kuitwa ABEL na baadae kuingia mafunzo ya kipaimara. Mdogo wao wa mwisho Kibada
alibatizwa na kuitwa YOHANA. Mwisho kabisa Babu
yetu Shekiboko naye akabatizwa na kuitwa HOKELAI.
Baada
ya Babu kubatizwa aliendelea vizuri katika imani ya Kikiristo na kulea watoto
wake vema. Akiwa mfugaji na mkulima.
Mwaka 1972 aliitwa mbinguni na baadae mwaka mmoja hivi bibi
Miriam naye aliitwa mbinguni.
Kwa shukrani za pekee kwa Mungu
ni kuwa tunaye Mzee Abel ambaye sasa ni mzee wa miaka 80 na kitu kwa Mujibu wa maelezo yake anasema
katika ukoo wetu baba/babu aliyebakia ni yeye tu kama
reference , akadai kuwa yuko mama mmoja dada yake yuko maeneo ya
upareni lakini hajulikani sana huku kwetu.mwanae mmoja dada yupo Mtae. Nimefanikiwa kumuona dada huyu.
FAMILIA YA KASINDA
Babu mkubwa wa kwanza anayeitwa
shekiondo ndiye anayewazaa wazee wetu
BOAZI NA YONA
Yona naye alipigana vita vya kumi
na nne.
BOAZI ndiye anayemzaa kaka
yetu marehemu Mganga Tamilwai,Kaka Izai, na Staile
YONA ndiye anayemzaa Pauli, Zephania (Mchungaji),Onai,Mkunde (sara),
na Otie
** Katika historia ya ukoo wetu yapo mambo
kadhaa yanajirudia kwa mfano
Babu aliyeitwa Mtambo ambaye jina lake baadae alipewa kaka Athumani mtoto
wa Mzee Hassani .Huyu Athumani(Mtambo) naye alipigana vita vya kumng’oa IDD Amini Dada wa Uganda. 1978-1979**
Aidha kwa Mujibu wa Mzee Abel ukoo wetu chanzo chake ni katika mji wa Lushoto eneo la Ubiri ambapo baadae ndugu walisambaa
katika maeneo mengi ya Lushoto kama Mtae,
Mambo ya Mtae, Dule ya Mlalo na Kwingineko
kama ilivyokuwa desturi ya Kabila la Wasambaa.
Itaendelea……….
** Tafadhali kama unayo taarifa/picha yoyote kuhusu ukoo wetu tafadhali nitumie niweke katika Blog yetu. Pia kila mtoto aliyepo sasa anaweza kuweka taarifa zake katika blog hii kwa maufaa ya wengine.
Na mwanafamilia Thomas Mgonda ( Joseph) Email: mgonda5@yahoo.com mobile: 0713600694
** Tafadhali kama unayo taarifa/picha yoyote kuhusu ukoo wetu tafadhali nitumie niweke katika Blog yetu. Pia kila mtoto aliyepo sasa anaweza kuweka taarifa zake katika blog hii kwa maufaa ya wengine.
Na mwanafamilia Thomas Mgonda ( Joseph) Email: mgonda5@yahoo.com mobile: 0713600694
Subscribe to:
Posts (Atom)